14.6 C
Nairobi
Thursday, August 5, 2021
Kenya
206,691
Total confirmed cases
Updated on August 5, 2021 5:33 am

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  VURUGU NA MAANDAMANO YANAENDELEA KUSHUDIWA MAREKANI

  Maelfu ya waandamanaji wamemiminika mtaani kote marekani huku maandamano ya amani
  ya kupinga mauawaji ya raia yanayofanywa na polisi yamegubikwa na machafuko ambayo
  yameikumba miji ya kuanzia philadelphia hadi Los angeles na kutokea pia nje ya Ikulu ya WhiteHouse.

  Maafisa wa majimbo wamechukua hatua mbalimbali ikiwa ni Pamoja na kuwapeleka maelfu ya
  wanajeshi wa ulinzi wa taifa,kuweka amri za kutokuwa nje usiku na kufunga mifumo ya kusafiri watu wengi ili kupungunza mavuguvugu ya maandamano lakini hayo hayakuzuia baadhi ya miji mingi kushuhudia vurugu.

  Maandamano hayo yaliingia siku ya sita jana baada ya kifo cha George Floyd mmarekani
  mweusi aliyeuawa na polisi mzungu aliyemkandamiza shingoni kwa kutumia goti huku akiwa
  amefungwa pingu mikononi mjini Minneapolis ..

  Siku mbili tu baada ya mkenya mmoja kwa jina Alex Nderitu kuandika ujumbe kwenye mtandao
  wa kijamii wa twitter akitishia kuwa waandamanaji sasa wanaenda kuchoma Ikulu ya white
  house pale ambapo ujumbe wake uliingia kwenye trending na kuleta wasiwasi katika Ikulu hiyo hadi pale Shirika la Ujasusi la Shirikisho la Marekani liliingilia kati na kufanya uchunguzi wao na kubaini kuwa Alex Nderitu yuko Nchini Kenya bali sio ilivyodhaniwa kwamba yuko karibu na
  Ikulu ya whiteHouse.

  Mkenya mwingine pia ameingia trending baada ya kuwaongoza waandamanaji kwa kuimba
  maneno ya Kiswahili ‘‘HAKI YETU’’ ambayo yanatumika sana kwenye maandamano yoyote
  Kenya.

  Maandamano hayo yamesambaa hadi mitaa ya London,Berlin na Oakland nchini New Zealand.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: