Kundi la madaktari wa kiasili limefuzu na shahada ya utabibu kutoka kwa chuo cha Utabibu wa Kiasili nchini Afrika Kusini.
Habari hii ilichapishwa kwenye mtandao wa Facebook na mmoja wa mahafala na kupakia picha zao za hafla ya mahafala baada ya kufuzu katika utabibu kutoka shule ya utabibu wa kiasili ya Afrika ya Mhlabuhlangene. Katika picha hizo, mahafala hao wanaonekana wakiwa wamevalia kanzu pamoja na mavazi ya kiasili na vipuli wakisimama wima kupigwa picha ya kufurahia hatua hiyo.
Shule hiyo ilibuniwa mwaka 1996 mjini Ladysmith, KwaZulu-Natal, na Profesa Sithembiso Calvin Shabalala. Shabalala, ambaye anasimamia masomo ya theolojia na kidini, pia amewakuza wanafunzi wengi ambao walimshukuru kwa kuwa nguzo katika kufuzu kwao.