16.1 C
Nairobi
Sunday, September 26, 2021
Kenya
248,392
Total confirmed cases
Updated on September 26, 2021 8:39 am

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  WAKENYA KUJIANDAA KWA MSIMU MREFU WA MVUA KUBWA KUANZIA MWEZI HUU WA AGOSTI

  Wakenya wametakiwa kujiandaa kwa msimu mrefu wa mvua kubwa mwezi huu wa Agosti.Katika utabiri wake wa kila wiki idara ya utabiri wa hali ya anga imesema mvua hiyo itanyesha kwenye maeneo ya juu ya Bonde la Ufa,Ziwa Victoria eneo la kati Kusini, eneo la Bonde la Ufa na Kaskazini Magharibi mwa nchi.

  Mvua hiyo itaendelea kuongezeka kati ya Agosti 6 hadi agosti 10.

  Aidha kutashuhudiwa mvua kubwa kwenye maeneo machache ya Kaskazini mwa Bonde la Ufa,Kaskazini Mashariki na Pwani ya Taifa.

  Mapema wiki hii Idara hiyo ilisema kuwa mvua Milimita 70 itanyesha kwenye kaunti za Samburu, Laikipia,Baringo,Elgeyo Marakwe, Pokot Magharibi,Trans nzoia,Uasin gishu na Nakuru.
  Utabiri huo wa kati ya tarehe 4 na tarehe 10 unaonyesha kuwa kaunti za Busia,Nandi,Kericho,Kakamega,Vihiga,Nyamira, Kisii,Bomet,Tharaka Nithi,Kisumu,Marsabit,Nyeri zitapokea Mililita 10 na 50 za mvua.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: