Polisi katika eneo la Rangwe katika kaunti ya Homabay wamewakamata washukiwa wawili wanaoshtumiwa kwa mauaji ya mwanaume mwenye umri wa miaka 28.Mauaji hayo yalifanyika katika kituo cha biashara cha Nyakuru katika eneo la Genga mnamo jumapili iliyopita .
Washukiwa Paul Owiti wa miaka 35 na Dennis Onyango wa miaka 28 wamekamatwa katika kijiji cha Otweyo huko Genga wakituhumiwa kumuua Joachim Hussein na kisha kuutupa mwili wake kando ya mto eneo hilo.
Mwili wake Hussein ulipatikana ukiwa na majeraha ya kukatwa kwa Panga.
Kwa mujibu wa mkuu wa polisi eneo la Rangwe Jane Sang’, uchunguzi wa mwanzo umewahusisha wawili hao waliokamatwa na mauaji ya Joachim. Hivyo wanasubiri kupelekwa mahakamani.