Mamlaka ya mawasaliano Tanzania TCRA imekifungia kituo cha runinga cha Wasafi kurusha matangazo yake kwa muda wa miezi sita kuanzia Leo tarehe 5,Januari 2021.
Hii ni baada ya runinga hiyo kukiuka kanuni za utangazaji kwa kurusha hewani kipindi cha maudhui yaliyomuonyesha msanii wa kutokea Tanzania Gift Stanford maarufu kama Gigy Money akionyesha utupu wake akiwa jukwaani.l
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Baraza la Sanaa la Tanzania(BASATA) ni kwamba kwa kufuata kanuni za Baraza la Sanaa Tanzania mwaka 2018, Baraza hilo limemfungia msanii huyo Gigy Money kwa miezi sita kutojishughulisha na shughuli zozote za muziki na kulipa faini ya shilingi za kitanzania Milioni moja.