19.4 C
Nairobi
Saturday, October 16, 2021
Kenya
251,669
Total confirmed cases
Updated on October 14, 2021 9:34 pm

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  WASHUKIWA WAWILI WA UHALIFU WANASWA WAKIWA NA SIMU 81 ZA WIZI

  Maafisa wa Usalama wamewakamata washukiwa wawili wa wizi jijini Kisumu nchini Kenya wakiwa na simu 81 za mkononi zinazoaminika kuibwa.

  Samuel Yassin mwenye umri wa miaka 27 na Daniel Chimota mwenye umri wa miaka 28 wamekamatwa katika chumba kimoja cha kukodisha jijini humo. Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi katika Kaunti ya Kisumu Ranson Lolmodooni, wawili hao ni wakaazi wa kaunti ya Kakamega na kwamba walikodisha chumba hicho Jumatatu wiki hii.

  Kamanda huyo wa polisi amesema kwamba usiku wa kuamkia jumatatu walilivamia duka kwa jina Kenshop Limited kwenye barabara ya Oginga Odinga na kupora simu hizo kabla ya kurejea katika chumba chao. Hivyo maafisa hao walifanikiwa kuwanasa wawili hao kupitia kamera za CCTV na kwamba watafunguliwa mashtaka asubuhi hii.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: