16.1 C
Nairobi
Sunday, September 26, 2021
Kenya
248,392
Total confirmed cases
Updated on September 26, 2021 8:39 am

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  WASIOJULIKANA WASHAMBULIA GEREZA NIGERIA

  Watu  wasiojulikana wameshambulia kwa silaha kali gereza lingine katika jimbo la Abia la Nigeria.

  Wafungwa wengi walitoroka wakati gereza hilo lilipokuwa likiteketezwa katika shambulizi hilo katika mkoa wa Bende, na hii kwa mujibu wa habari kwa vyombo vya habari vya kitaifa.

  Mashambulizi mbalimbali hufanyika mara kwa mara likiwemo la Aprili 5, 2021, ambapo Idara ya Magereza nchini Nigeria ilithibitisha kuwa wafungwa 1,844 walitoroka na magari 50 yalichomwa moto katika gereza la Owerri katika mji mkuu wa jimbo la Imo.

  Hata hivyo,vituo kadha vya polisi vimeshambuliwa nchini Nigeria tangu Januari Mwaka huu.Wavamizi hao pia wamekuwa wakiiba idadi kubwa ya bunduki katika mashambulio hayo.

  Aidha, mashambulizi mengi kama hayo yamekuwa yakibainika kufanywa na kundi linalojitenga la Biafra (IPB) kusini mwa Nigeria.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: