16.1 C
Nairobi
Sunday, September 26, 2021
Kenya
248,392
Total confirmed cases
Updated on September 26, 2021 8:39 am

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  WATU 14 WAFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI LA KUTUMIA NYAYA (CABLE CARS) ITALIA

  Watu kumi na wanne wafariki dunia na mtoto mmoja kujeruhiwa baada ya gari ya kutumia Nyaya kuanguka mlimani karibu na Ziwa Maggiore Kaskazini mwa Italia Jumapili Mei 23.

  Picha ya ajali ya gari ya kutumia nyaya

  Ajali hiyo imetokea wakati gari hilo lilikuwa linasafirisha abiria kutoka mji wa mapumziko wa Stresa kwenda Mlima wa Mottarone ulioko eneo la Piedmont.

  Kulingana na maafisa wa uokoaji wa Alpine,walikuwa wameweka wazi kupitia kwa mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa idadi ya waliofariki dunia katika ajali hiyo ilikuwa watu kumi na watatu na watoto wawili kupata majeraha mabaya.Ambapo baadae iliwekwa wazi kuwa mtoto mmoja kati ya waliojeruhiwa ameaga dunia huku akipokea matibabu hospitalini.

  Hata hivyo, huduma ya gari za kutumia nyaya eneo hilo zilianza mwaka 1970. Mwaka 2014 na 2016 huduma za gari hizo zilisitishwa kwa ajili ya kufanyiwa ukarabati au kutengenezwa kisha kuruhusiwa kuendelea na huduma.

  Chanzo cha ajali hiyo bado hakijawekwa wazi na mamlaka au kampuni husika.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: