14.6 C
Nairobi
Thursday, August 5, 2021
Kenya
206,691
Total confirmed cases
Updated on August 5, 2021 6:33 am

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  WATU 45 WAFARIKI DUNIA KWENYE MKANYAGANO KATIKA UWANJA WA UHURU DAR ES SALAM,TANZANIA

  Idara ya Polisi nchini Tanzania imethibitisha kuwa watu 45 walifariki dunia katika mkanyagano wakati wa kutazama mwili wa hayati Rais Magufuli katika Uwanja wa Uhuru ulioko jijini Dar es salaam nchini humo.

  Kisa hicho cha kuhuzunisha kilitokea siku ya pili wakati wakazi walijitokeza kwa wingi kutoa heshima zao za mwisho kwa Hayati raid wao katika uwanja huo Jumapili, Machi 2, 2021. Kamanda wa Polisi wa Dar es Salaam.

  Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi limesema liliongea na Lazaro Mambosasa ambaye pia alithibitisha kuwa waombolezaji wengine 37 waliwachwa na majeraha. “Hawa watu si wahalifu. Walikwenda uwanjani kuonyesha upendo kwa kiongozi wao lakini kwa sababu ya idadi kubwa ya watu, baadhi yao walikosa subira na kuamua kutumia njia mbaya kuingia uwanjani na ndivyo tatizo lilitokea,” aliongeza.

  Hata hivyo wiki iliyopita, miili ya watu watano wa familia moja ambao pia waliangamia kwenye mkanyagano huo katika Uwanja wa Uhuru ilizikwa. Susan Mtuwa na wanawe wawili Nathan (6) na Natalia (5) walizikwa pamoja na watoto wengine wa shemeji yake, Chris (11) and Michelle (8).

  Rais John Magufuli aliyetangazwa kufariki Machi 17,2021 kutokana na matatizo ya moyo, alizikwa wilayani Chato Mkoa wa Geita siku ya Ijumaa, Machi 26,2021.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: