14.6 C
Nairobi
Thursday, August 5, 2021
Kenya
206,691
Total confirmed cases
Updated on August 5, 2021 7:33 am

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  WATU 9 WAFARIKI KWA AJALI YA BARABARANI GILGIL

  Watu 9 wamepoteza maisha kwa ajali ya barabarani baada ya matatu waliyokuwa wakisafiria kugongana ana kwa ana na trela Ijumaa Februari 12 asubuhi.

  Ajali hiyo ilifanyika katika eneo la Gilgil,barabara ya Nakuru-Nairobi karibu na hospitali ya St Mary’s na tisa hao waliripotiwa kufariki papo hapo. Kamanda wa polisi eneo la Gilgil John Onditi alisema ajali hiyo ilifanyika saa kumi na moja alfajiri wakati matatu hiyo ilikuwa ikielekea jijini Nairobi. Walioshuhudia walisema trela hiyo ilijaribu kulipita gari lingine na kukutana na matatu hiyo ambapo ziligongana ana kwa ana.

  Imethibitishwa kuwa pia matatu hiyo ilikuwa imebeba abiria kuzidi idadi inayohitajika kulingana na sheria za covid 19.

  Mbunge wa Molo Kuria Kimani alisema walioangamia ni wafanyibiashara kutoka Molo waliokuwa wakielekea soko la Gikomba kuchukua bidhaa.

  “Matatu iliyokuwa ikielekea Nairobi kutoka Molo ikiwa na wafanyibiashara waliokuwa wakielekea Gikomba ilihusika katika ajali ya barabara eneo la Mbaruk ambapo watu kadhaa walifariki,” Kuria alisema.

  Kwa mujibu wa ripoti za polisi,mtoto wa miaka mitano ni baadhi ya walionusurika mauti wakati wa ajali hiyo huku akipata majeraha tu madogo.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: