19.4 C
Nairobi
Saturday, October 16, 2021
Kenya
251,669
Total confirmed cases
Updated on October 14, 2021 9:34 pm

SARAH OBAMA, BIBI YA RAIS WA ZAMANI BARACK OBAMA AFARIKI DUNIA

Sarah Obama, bibi ya Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, amefariki dunia katika Hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu akiwa na miaka...
More

  Latest Posts

  YOWERI MUSEVENI NDIYE RAIS MTEULE UGANDA

  Tume ya Uchaguzi ya Uganda imemtangaza rais aliye madarakani Yoweri Museveni mshindi wa Uchaguzi Mkuu wa 2021. Tume hiyo ilisema Yoweri, mwenye umri wa miaka 76, aliwashinda wagombea wengine 10 wa urais na kuongeza muda wa utawala wake wa miaka 35 kwa muhula mwingine hadi 2026 baada ya kujizolea kura nyingi.

  Rais mteule Museveni alipata asilimia zaidi ya 50% kwenye uchaguzi, EC inamtangaza mgombea Yoweri Tibuhaburwa Kaguta Museveni kama rais wa Uganda kupitia uchaguzi uliofanyika Januari 14, ” mwenyekiti wa tume hiyo Simon Byabakama alisema. Matokeo ambayo yalitangazwa dakika chache kabla ya saa 4 jioni Jumamosi, Januari 16, yalionyesha jumla ya kura 10,359,479 zilipigwa katika kura ya Januari 14 ambapo kura halali zilikuwa 9,978,093. Museveni ambaye aliwania urais kwa tikiti ya chama cha National Resistance Movement, alikuwa kifua mbele tangu siku ya kwanza kura zilipoanza kuhesabiwa na hadi anatangazwa mshindi kwa kura 5,851,037.

  Ushindi huo ulitafsiriwa kuwa asilimia 58.64% ya jumla ya kura zilizopigwa, mpinzani wake wa karibu Robert Kyagulanyi almaarufu Bobi Wine alipata kura 3,475,298 (34.83%) ambapo atazidi kusalia katika upinzani. Akizungumza na waandishi wa habari mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 38 alidai matokeo ya uchaguzi huo hayakuwa ya kweli na kwamba alikuwa mwathiriwa wa utapeli.

  Latest Posts

  Don't Miss

  Stay in touch

  To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

  %d bloggers like this: